TIC YAHAMASISHA WADAU KUJA KUWEKEZA MKOANI DODOMA

0
54

Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, wakipatiwa maelezo na Mtendaji Mkuu wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Clifford Tandari, juu ya fursa za uwekezaji zilizopo Mkoani Dodoma, wakati wa Mkutano Mkuu wa Uwekezaji wa Dunia kanda ya Afrika uliofanyika Mjini Kigali nchini Rwanda hivi karibuni. Mkutano huo uliandaliwa na COMESA kwa kushirikiana na Serikali ya Rwanda.

Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, wakimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Clifford Tandari, alipokuwa akiwaelezea juu ya fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Mkoani Dodoma, wakati wa Mkutano Mkuu wa Uwekezaji wa Dunia kanda ya Afrika uliofanyika Mjini Kigali nchini Rwanda hivi karibuni.