ZAIDI ya ekari 300 za mpunga zaharibiwa na ndege aina ya kwelea kwelea

0
70

ZAIDI ya ekari 300 za mpunga katika kata ya Kahe wilaya Moshi mkoani Kilimanjaro zimevamiwa na ndege aina ya kwelea kwela na kuathiri vibaya mazao ya wakulima.

Diwani wa kata hiyo Rodrick Mmanyi alisema kuwa ndege wameathiri kwa kiwango kikubwa mazao ya wakulima

ambao walikuwa wako katika harakati  za kuvuna mazao yao.

Amesema  ndege hao wamevamia mashamba hayo wiki iliyopita ambapo mpakasasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na  Halmashauri ya wilaya Moshi vijijini kuwadhibithi ndege hao wasiendelee kuathiri mazao ambapo  zaidi ya wakulima 1000 mazao yao yameharibiwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti wakulima wameiomba Serikali kuwasiadia ili kuwa nusuru na janga la njaa kutokana na kwamba mazao yao yote yameliwa na ndege