Ushirikiano wa sekta ya ulinzi kati ya Kenya na Jordan

Mfalme wa Jordan Abdullah II ametekeleza ziara yake nchini Kenya kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya ulinzi.

Katika ziara hiyo, Mfalme Abdullah II alipokewa na kukaribishwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kuelekea katika kambi ya Embakasi jijini Nairobi.

Viongozi hao wawili walihudhuria zoezi la kijeshi la ‘Swift Eagle’ lililoendeshwa na kikosi cha jeshi la KDF na kuonyesha mbinu za kukabiliana na ugaidi.

Viongozi hao walishuhudia zoezi hilo wakiwa wamevalia magwanda ya kijeshi na baadaye wakatia saini mkataba wa ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Ziara hiyo ya Mfalme Abdullah ilikuwa ni ya kwanza tangu mwaka 1999 alipoingia madarakani.