Somalia yatangaza kufanya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba tarehe 30 huku uchaguzi wa wabunge ukianza mwezi ujao.

Taarifa hiyo ilitolewa na shirika la habari la Ufaransa la AFP siku ya Jumatatu.

Timu ya tume ya uchaguzi ya FIEIT inayofadhiliwa na UN ilikutana na viongozi miongoni mwao akiwa rais wa Somalia Hassan Sheik Mohamud .

FEIT ilithibitisha rasmi kuwa uchaguzi wa wabunge utafanyika kati ya Septemba 24 hadi Oktoba 10 .

Aidha orodha ya wagombea wa urais itabainishwa hivi karibuni huku rais Mahmud kugombea kiti hicho kwa awamu ya pili.

Somalia ilizama katika vita mnamo mwaka 1991 baada ya mababe wa vita kupindua rais wa wakati huo Mohamed Siad Barre .

Wakati Somalia inajitayarisha kufanya uchaguzi mkuu wa 25 katika historia yake ya demokrasia tishio la usalama bado ni changamoto kuu kutoka kwa wanamgambo wa Al Shabaab.