Tanzania imeeleza kwamba
juhudi za serikali ya awamu ya  Tano za
kukabiliana na  vitendo vya rushwa  hazitaweza kufanikiwa   kama
havita ungwa mkono na  jumuiya ya
kimataita.
Ni kwa sababu hiyo, Tanzania, inazitaka nchi
zilizoendelea kuwawajibisha wawekezaji wao na makampuni yao ili  yalipe kodi.
Hayo yameelezwa jana  jumatatu na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Dkt. Agustine Mahiga ( Mb)  wakati
alipolihutubia  Baraza Kuu la 71
la Umoja wa Mataifa na kutumia  fursa
hiyo kuelezea vipaumbele vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Mahinga akafafanua kwamba, lengo namba
kumi na sita la  maendeleo endelevu
linatambua kuwa,  rushwa inakandamiza
juhudi za kumbana na  umaskini na   usawa wa jinsia,  inazuia
fursa na inakuwa na kama kodi kwa familia maskini pale wanapotafuta  haki.
Ni katika muktadha  huo,   akasema, serikali  ya
Tanzania imeamua kuanzisha vita dhidi ya rushwa  kwa kuhuisha uwazi, uwajibikani  na usahihi katika utoaji wa huduma  kwenye taasisi za  umma.
Akasisitiza kwamba
serikali  imeweka misingi mizuri ya  uwajibikaji inayomtaka mtumishi wa umma
kutambua kwamba  wajibu wake wa kwanza
ni  kutoa huduma bora na kwa wakati kwa
umma.
“Juhudi hizi za serikali za kupambana na rushwa
hazitaweza kuzaa matunda bila ya
kuungwa mkono wa jumuiya ya kimataifa. Nchi zilizoendelea zinatakiwa  kuwawajibisha wawekezaji wao  pamoja na makampuni yao ili  waweze kulipa kodi stahiki.” Akaeleza
zaidi  Waziri  Mahinga
Na  kuongeza. “Ni lazima wawe tayari kurudisha
mali na fedha  zilizoibwa kutoka nchi
zinazoendelea na kuzificha katika nchi zao ili mali  na fedha hizo ziweze kusaidia maendeleo  yetu”.
Kuhusu fursa za jinsia
na uwezeshwaji wa wanawake,  Waziri  Mahinga ameelezea juhudi mbalimbali ambazo
zimefanywa na serikali katika
kuwawezesha  wawanake ikiwamo
kushika ngazi za juu za maamuzi kuanzia serikali kuu  hadi bunge na uwezeshwaji wa  kiuchumi.
katika kudhibitisha
kuwa Tanzania  inazingatia usawa wa
jinsia katika uteuzi wa ngazi  mbalimbali
za maamuzi,  Waziri Mahinga  ameeleza kwamba kwa mara ya kwanza  wakati wa
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,  Rais
John Pombe Magufuli  alimchangua
mwanamke  kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
“Uteuzi  huu
unathibitisha nia ya nchi yangu ya kuona wanawake  wengi zaidi wanakuwa katika   nafasi za ngazi za  juu  za
maamuzi. Na ajenda hii ya uwezeshwaji wa wanawake wa Tanzania sasa inamilikiwa
na wanawake wenyewe” akasisitiza  Waziri
Kwa upande wa vijana, Kiongozi huyu wa Ujumbe
wa Tanzania ambaye amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  amesema.
Vijana ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote lile, siyo tu
kwamba ni viongozi wa kesho lakini pia ni viongozi wa sasa.
Akatahadharisha kwamba
kwa  kutowapa kiupaumbele vijana  ni kujitafutia  matatizo makubwa kutokana na kile alichosema ni
rahisi  kurubuniwa na makundi ambayo ni
hatari kwa ustawi wa jamii na taifa .
“ Kutoka na  kwamba idadi ya vijana ni kubwa,  serikali inachukua hatua mbalimbali za  kuliwezesha kundi hili la jamii ambalo ni muhimu
katika utekelezaji wa ajenda 2030. Na ili
vijana   waweze kutekeleza  jukumu hilo  serikali imeanzisha  mfuko wa maendeleo wa  vijana mfuko ambao hadi mwezi March mwaka huu
jumla ya  shiling 1.6 bilioni
zilipelekwa  kwa vikundi 284 ya  vijana”.
Kuhusu elimu,
eneo ambalo ni kipaumbele kingine cha Tanzania,   Waziri ameeleza kuwa   upatikanaji wa elimu jumuishi  na ya viwango ndicho kipaumbele cha serikali
kwa  kuwa    Serikali inaamini kuwa, elimu ni  ni nyenzo muhimu   kwa maendeleo endelevu
Akafafanua  kwamba
serikali  inatekeleza bila kuchoka
kuhakikisha kwamba  watoto wote wa kike
na wa kiume wanapata  elimu bure kuanzia
shule ya msingi hadi sekondari. Pamoja na kutoka   elimu
bure, serikali imeboresha mitaala yake kwa kuzingatia mahitaji ya karne ya 21.
“Alipoingia
madarakani,  Mhe.  John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania alitangaza kwamba   kuanzia elimu ya msingi  hadi sekondari itakuwa bure. Serikali  imetenga zaidi ya  shilingi 263 bilioni ili kuhakikisha
elimu  inakuwa bure kwa wote.
Vipaumbele vingine
vya  Tanzania ambavyo Mhe. Waziri
amevianisha katika  hotuba  yake ni pamoja na  mikakati ambayo  serikali imejiwekea  katika utekelezaji wa mkataba wa mabadiliano
ya tabia nchi ( Paris Agreement),
utekelezaji wa   malengo ya
maendeleo endelevu ( agenda 2030), mapambano dhidi ya  dawa haramu za kulevya,  na
kukabiliana na  ugaidi ambao  amesema  ni
tatizo ambalo linaendelea kukua na kuwa tishio  hata kwa  nchi za Afrika Mashariki.
Kwa upande wa
utekelezaji wa  agenda 2030, Waziri
amesema agenda hiyo imeanishwa  katika
mipango ya kitaifa ya  miaka  mitano ya
maendeleo  kwa pande zote za
muungano.  Hata hivyo  amesema kuwa Tanzania  imebaini kwamba haitaweza kukamilisha
kwa  wakati agenda 2030 pasipo
kushirikiana na wadau  mbalimbali  wa maendeleo.
Kuhusu  migogoro inayoendelea katika nchi za Burundi
na  Sudani ya Kusini, Waziri Mahiga
amezitaka pande zote zinazopingana  nchi
Burundi kutambua kwamba majadiliano ambayo ni jumuishi kwa pande zote
ndiyo  njia sahihi ya kutatua matatizo ya
nchi yao.
Kwa upande wa Sudani ya
Kusini,  Waziri  amesema Tanzania inaungana na   nchi nyingine kulaani matukio ya hivi
karibuni ya kujirudia kwa machafuko nchini humo.

Ameongeza kuwa,  Tanzania ambaye ni  Mwenye -Kiti wa sasa wa  Jumuiya ya
Afrika Mashariki,  iliitisha kikao
kisicho cha kawaida ili  kuzungumzia hali
ya kisiasa ya Burundi na Sudani ya Kusini. “
Tunatumaini kwamba nchi  zote
mbili  zitaweka maslahi  ya wananchi wao mbele ili kumaliza
machafuko”.

Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa  Afrika Mashariki pia
aligusia kuhusu marekebisho ya mfumo wa   Baraza
Usalama la Umoja wa Mataifa,  ili
liwe jumuishi.

Na Mwandishi Maalum,
New York