MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Mehboob Manji ameipa klabu hiyo eneo la ekari 715 lilipo Geza Ulole, Kigamboni, Dar es Salaam.Wasaidizi wa Manji wamekabidhi eneo hilo leo mchana katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Maofisa wa chama na Serikali ya Kigamboni.

Aliyepokea eneo hilo kwa niaba ya klabu ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu, Mama Fatma Karume aliyeambatana na Mjumbe mwingine wa Bodi hiyo, Dk. Jabir Idris Katundu, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu, Samuel Lukumay na Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit.

Sasa rasmi utafanyika ujenzi wa uwanja na uwekezaji mwingine katika eneo hilo lililobatizwa kijiji cha Yanga SC.

Na , Clement Shari