Mwanamke matatani kwa kauli ya chuki dhidi ya Uislamu Denmark

Mwanamke mmoja aliyetoa kauli ya chuki dhidi ya Uislamu baada ya mashambulizi kutekelezwa kwenye msikiti nchini Denmark ameripotiwa kutozwa faini ya fedha Kron 3,000 (takriban Euro 400).

Kulingana na maelezo yaliyotolewa na mahakama ya mji wa Herging, mwanamke huyo alitozwa faini kwa kuzingatia kifungu cha kanuni 136 baada ya kuandika ujumbe mtandaoni  unaosoma ‘Nitatoa lita moja ya mafuta!’

Ujumbe huo aliotoa mwanamke huyo kwenye mtandao wa jamii ulikusudia kuukejeli na kuteketeza msikiti ulioshambuliwa.

Baada ya kutozwa faini na mwendesha mashtaka Linette Lysgaard pamoja na kuhukumiwa kifungo cha siku 60 gerezani, mwanamke huyo alizungumza na televisheni ya TV2 na kuomba radhi kwa kauli hiyo.

Mnamo mwaka jana, msikiti mmoja wa mji kuu wa Copenhag nchini Denmark ulishambuliwa na baadaye kukaanzishwa kampeni ya kuchangia mafuta kwenye mitandao ya jamii kwa ajili ya kuuchoma moto.

Kwingineko wiki mbili zilizopita, shule ya Mina Hindholm inayomilikiwa na muungano wa Kiislamu nchini Denmark pia ilishambuliwa kwa bomu na kukumbwa na uharibifu mkubwa.