Ndege ya Cristiano Ronaldo yapata ajali mjini Barcelona nchini Uispania

Ndege aina ya Gulfstream G200  ya mshambuliaji nyota timu ya Real Madrid ya Uispania na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo yafanya ajali bila kuleta madhara yoyote kwa abiria wakati wakutua katika uanja wa ndege mjini Barcelona nchini Uispania.

Kwa mujibu wa habari zilizotolewa zinafahamisha ya kwamba ajali hiyo ilitokea baada ya ndege hiyo kupata tatizo la kiufundi na kusababisha rubani  kukushindwa kutua vizuri.

Ifahamike ya kwamba Ronaldo hakuwemo ndani ya ndege hiyo wakati wa ajali hiyo.