Kim Kardashian avamiwa na kuibiwa jijini Paris

0
30

Kim Kardashian avamiwa na kuibiwa jijini Paris

Watu waliovalia kama polisi walivamia chumba cha hoteli alimokuwa nyota wa Marekani wa  vipindi aina ya ‘Reality Show’ za televisheni Kim Kardashian na kumuibia mamilioni ya euro pamoja na vito.

Msemaji wa msanii huyo mashuhuri alisema kuwa Kim alitikiswa na tukio hilo inagawaje hakujeruhiwa .

Watu hao waliojificha kwa kuvaa mavazi ya polisi waliripotiwa kuingia katika chumba cha hoteli cha Kim Kardashian na na kumtishia kwa bunduki.

Mumewe Kardashian,Kanye West  alisitisha tamasha la muziki lililokuwa limeandaliwa jijini New York na kusema kuwa ilikuwa ni ‘Dharura ya kifamilia ‘.

Kardashian ni mojawapo ya watu mashuhuri muhimu wanaotambulika sana Marekani nakwa muda sasa amekuwa akionekana katika wiki ya mitindo mjini Paris .