Polisi Dar yamnasa mtuhumiwa sugu wa ujambazi

0
30

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni jambazi sugu katika maeneo ya Goba nje kidogo ya Jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna wa Polisi Simon Sirro ametoa taarifa hiyo wakati akitoa taarifa ya kukamatwa mtu huyo aitwaye Musa Katera ambaye ni mfanyabiashara akiwa na bastola aina Browning, magazine mbili pamoja na risasi 11.

Katika tukio lingine Jeshi la Polisi limeanza doria maalum katika maeneo ya Buguruni ili kubaini kikundi cha watu kinachoendesha zoezi la uhalifu wa kuwatoboa macho watu.

Wakati huohuo kikosi cha usalama barabarani Kanda Maalaum ya Dar es Salaam kimekusanya shilingi 464,790,000 kupitia tozo za makosa ya usalama barabarani ndani ya siku kumi kutokana na makosa 15,493 ya barabarani.