Reli ndefu zaidi Afrika ya treni za umeme yazinduliwa Ethiopia

0
30

Waziri mkuu wa Ethiopia azindua rasmi reli ndefu zaidi Afrika ya treni za umeme katika mji mkuu wa Addis Ababa

Ethiopia imezindua reli ndefu zaidi Afrika ya treni za umeme inayounganisha mji mkuu wa Addis Ababa, Djibouti na miji mengine ya bandari.

Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn pamoja na rais wa Djibouti Ismail Omar Gulle walihudhuria kwenye hafla ya uzinduzi wa reli hiyo ambayo ni ya kwanza barani Afrika.

Desalegn alitoa hotuba ya ufunguzi na kusema kwamba reli hiyo ya treni za umeme itasaidia kukuza sekta za uchumi na biashara kati ya Ethiopia na Djibouti.

Maelezo zaidi yanaarifu kwamba reli hiyo itawezesha wafanyabiashara wa Ethiopia na Djibouti kusafirisha bidhaa zao kwa muda wa masaa 10 kati ya nchi hizo.

Desalegn pia alitoa shukrani na kuwapongeza wahandisi na wafanyakazi wote waliohusika kwenye ujenzi wa mradi huo, na kufahamisha matumaini yake ya kuchangia maendeleo zaidi barani Afrika.

Mradi huo wa reli ya treni za umeme ulitekelezwa na serikali ya China na baadaye unatarajiwa kupanuliwa hadi miji mengine.