Vikosi vya Simba na Mbeya City vitakavyoanza leo

0
28

Simba wanawavaa wenyeji wagonga nyundo wa jiji la Mbeya, Mbeya City FC katika mchezo utakaonza saa 10:30 jioni katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku mshambuliaji wake wa kimataifa Laudit Mavugo kutoka Burundi na mlinzi Jjuko Murshid kutoka Uganda wakianiza benchi.

Kikosi cha Simba kinachoanza kina mabadiliko ya nafasi moja tu, na kile kilichoanza katika mchezo dhidi ha watani waonwa jadi Yanga, mchezo ukiomalizika kwa sarw ya bao 1-1.

Fredrick Blagon anachukua nafasi ya Laudit Mavugo, huku kiungo Joans mkude aliyetolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 26 katika mchezo uliopita dhidi ya Yanga, akiendelea kuvaa kitambaa cha unahodha katika mchezo wa leo.

Upande wa wenyeji Mbeya City wanaonolewa na kocha mmalawi, Kina Phiri hakina mabadiliko makubwa zaidi, kufuatia kiungo Ramadhan Chombo kumpisha Joseph Mahundi katika kikosi kinachoshuka kuwakabili Simba jioni ya leo.

Simba SC XI: Angban- Bokungu, M Hussein, Lufunga, Mwanjale; Mkude, Kichuya, Mzamiru; Blagnon, Ajibu, Kazimoto.
Subs: Manyika, Banda, Jjuko, Ndemla, Mo Ibrahim, Mavugo, Ame Ally.

Mbeya City XI: Chaima, Kabanda, Kerenge, Tumba, Zahir; Mkandawile, Mahundi, Kenny; Omary, Ralpha, Nchimbi
Subs: Fikirini, Mwangosi, Mlawa, Chombo, Hamidu, Rutabonzye