Mshukiwa wa ugaidi ajitoa uhai gerezani Ujerumani

0
28

Jaber Albakr ajitoa uhai gerezani baada ya kukamatwa alipokuwa akijiandaa kuendesha shambulizi la kujitoa mhanga nchini Ujerumani

Mshukiwa wa ugaidi Jaber Albakr ameripotiwa kujitoa uhai gerezani baada ya kukamatwa alipokuwa akijiandaa kuendesha shambulizi la kujitoa mhanga nchini Ujerumani.

Jaber Albakr ambaye ni raia wa Syria, alitiwa mbaroni na vikosi vya usalama alipokuwa katika maandalizi ya kuendesha shambulizi la kujitoa mhanga na kuzuiwa kwenye gereza la Leipzig.

Jaber Albakr mwenye umri wa miaka 22 na aliyekuwa mhamiaji aliyetafuta hifadhi Ujerumani, alikamatwa mwishoni mwa juma na kutupwa gerezani.

Kulingana na vyanzo vya shirika la habari la DPA, Jaber Albakr alisemekana kuanzisha mgomo wa njaa baada ya kufungwa gerezani.

Hata hivyo bado hakuna maelezo yoyote ya wazi yaliyotolewa kuhusiana na njia aliyotumia Jaber Albakr kujitoa uhai ndani ya gereza hilo maalum alilokuwa akizuiwa kwa madai ya ugaidi.

Mahakama inasisitiza kwamba mshukiwa huyo alikuwa akishirikiana na kundi la DAESH kwa ajili ya utekelezaji wa mashambulizi.