Donald Trump akumbwa na kashfa nyingine Marekani

0
25

Mwanamke mmoja amshutumu Donald Trump kwa kumnyanyasa kijinsia miaka ya 1990

Mgombea urais wa chama cha Republicans Donald Trump, amekumbwa na kashfa nyingine ya unyanyasaji wa kijinsia nchini Marekani.

Mwanamke mmoja aitwaye Kristin Anderson anayeishi California, alimshutumu Trump kwa kuwahi kumnyanyasa kijinsia mjini New York miaka ya 1990 baada ya kukutana kwenye mgahawa wa burudani nyakati za usiku.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 46 alitoa maelezo kwa wanahabari wa gazeti la Washington Post na kutoa tuhuma hizo za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya Trump.

Maelezo zaidi yanaarifu kwamba Trump alitumia utajiri wake katika miaka hiyo kuwanyanyasa wasichana wadogo kama vile Anderson aliyekutana naye akiwa na umri wa miaka 20 wakati huo.

Katika siku za hivi karibuni, Trump amekuwa akikashifiwa kwa kesi za unyanyasaji na kauli za udhalilishaji dhidi ya wanawake nchini Marekani.