Pacha walioshikana kiwiliwili wazaliwa Bangladesh

0
24

Watoto wawili pacha walioshikana kiwiliwili wazaliwa katika hospitali moja ya mji wa Dakka nchini Bangladesh

Watoto wawili pacha walioshikana kiwiliwili wameripotiwa kuzaliwa katika hospitali moja ya mji mkuu wa Dakka nchini Bangladesh.

Mwili wa pacha hao walioshikana umebainishwa kuwa na vichwa viwili, mikono mine na miguu minne.

Baada ya watoto hao kuzaliwa, walihamishiwa katika kitengo maalum cha uzazi cha hospitali hiyo.