NDALICHAKO:Wasiorejesha mikopo wanakwamisha juhudi za kutoa mikopo kwa wanavyuo

0
33

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa JOYCE NDALICHAKO amesema kuwa nia njema ya serikali ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu inakwamishwa na kasi ndogo ya urejeshwaji wa mikopo hiyo.

Profesa NDALICHAKO amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2005 hadi Juni mwaka 2016 serikali imetoa mikopo ya zaidi ya Shilingi Trioni Mbili Nukta Tano kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu mbalimbali nchini, lakini  fedha zilizorejeshwa hadi sasa ni takribani Shilingi Bilioni 147  tu.

Profesa NDALICHAKO ametoa kauli hiyo wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 40 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi – CCM lililofanyika Mjini KIGOMA.