Watumishi wa umma washauriwa kujiendeleza kielimu

0
79

Waziri Mkuu Mstaafu MIZENGO PINDA amewashauri wakuu wa mikoa kuwahamasisha wananchi na watumishi wa umma kujiendeleza kielimu kupitia elimu masafa inayotolewa na ChuoKikuu huria nchini kwa lengo la kuboresha fanisi kazini.

Akizungumza na wanafunzi na viongozi wa Chuo Kikuu Huria Kituo cha
IRINGA, PINDA amesema wakuu hao wa mikoa wawahimize watumishi wa serikali za mitaa kutumia fursa hiyo kwani mfumo wa chuo  hicho unamrahisishia mwanafunzi kusoma akiwa anaendelea na kazi.

PINDA ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu huria amesema elimu inayotolewa na chuo hicho ubora wake uko sawa na elimu inayotolewa kwenye vyuo vingine vya elimu ya juu nchini ambapo wamewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kusoma kwenye chuo hicho.

Waziri Mkuu Mstaafu PINDA ametembelea chuo hicho kwa mara ya kwanza kwa lengo la kujua changamoto zinazokikabili chuo hicho na kuzitafutia ufumbuzi.