Afisa elimu PWANI atakiwa kuweka utaratibu wa kukutana na wananchi na wazazi .

0
58

Waziri wa Elimu, Sayansi na teknolojia, PROF JOYCE NDALICHAKO amemuagiza Afisa Elimu wa mkoa wa PWANI, JERMANA MNG’AHU kuweka utaratibu wa kukutana na wananchi wazazi na wadau wa elimu kuzungumzia maendeleo ya elimu mkoani humo.

Waziri NDALICHAKO ametoa agizo hilo kutokana na kutofurahishwa na matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ya mwaka jana wakati akizungumza na viongozi wa wilaya ya RUFIJI na wanafunzi wa shule za sekondari za IKWIRIRI, MUHORO na UTETE.

PROF.NDALICHAKO pia amewataka wazazi kuacha kuwashirikisha watoto katika masuala yasiyohusiana na elimu ili waweze kuzingatia masomo yao na kufaulu kwenye mitihani yao mbalimbali.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa mkoa wa PWANI,  JERMANA MNG’AHU amewataka wanafunzi moani humo kuacha kuendelea baadhi ya mila na desturi potofu zinachangiakuwafanya wakatishe masomo yao.