jeshi la polis kanda maalum ya dar es salaam limewakamata watu 257 kwa tuhuma za kujiusisha na ulanguzi na utumiaji wa dawa za kulevya.

0
98

 

hayo yamethibitishwa mbele ya wanahabari hii leo mjini dar es salaam na kamanda wa jeshi la polis katika kanda hio maalum saimon siro.

watu hao wamekamatwa katika msako maalumu ambao ni endelevu kwaajili ya kupambana na kutokomeza ulanguzi wa dawa za kulevya pamoja na utumiaji hapa nchini.

AUDIO:hapa ni kamishina saimo siro

.DSC_7326

katika hatua nyingine kamishina siro amesema jeshi hilo la polisi limekamata pikipiki 1280 kutokana na makosa mbalimbali likiwemo la kufanya safari katika barabara ya magari yaendeyo kasi BRT.
Jumla ya milioni 460 zimepatikana kutokana na tozo za makosa mbalimbali yanayofanywa na vyombo vya moto barabarani kwa muda wa juma moja lililopita mjini dar es salaam.