Mkuu wa mkoa wa Kigoma apiga marufuku wanawake kudhulumiwa

0
105

Mkuu wa mkoa wa wa KIGOMA Brigedia Jenelari  Mstaafau EMMANUEL  MAGANGA  amepiga marufuku vitendo vya baadhi ya wanaume  mkoani humo kuwadhulumu na kuwatishia kuwafukuza wanawake pindi wanapodhubutu kutetea haki zao.

Akifunga maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani humo MAGANGA amesema na badaala kuendeleza vitendo hivyo washirikiane nao kutambua na kuchangamkia fursa za maendeleo zilizopo nchini.

Mapema akimkaribisha mkuu huyo wa mkoa kuzungumza katika maadhimisho hayo  mkuu wa wilaya ya Kakonko  kanali hosea NDAGALA amewataka wanawake wilayani humo kujiunga kwenye vikundi  mbalimbali vya ujasiriamali.