Maelfu wajipanga kuandamana Afrika Kusini

0
25

Maelfu ya raia wa Afrika Kusini, wakiwamo viongozi wa vyama vya upinzani, taasisi za kiraia na wanaharakati wanatarajia kufanya maandamano kumshinikiza Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma, ajiuzulu.

Maandamano hayo yataanzia katika Mnara wa Kanisa, Pretoria, hadi katika eneo la Union Building.