Msambatavangu aachiwa kwa dhamana

0
53

Mahakama ya mkazi mkoa wa Iringa imemuachia huru kwa dhamana aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu (41) baada ya kukana shtaka linalomkabili. Akisoma shauri hilo wakili wa Serikali , Alex Mwita alisema Msambatavangu anashtakiwa kwa kosa la kumshambulia Neema Nyongole mnamo Februari 17 mwaka huu maeneo ya Kibwabwa kinyume na kifungu cha sheria namba 240 cha mwaka 2002. Baada ya mshtakiwa kusomewa shtaka hilo mahakamani hapo, alikana kutenda kosa hilo na kusema sio kweli. Wakili Mwita alisema kuwa upelelezi wa shtaka hilo bado unaendelea huku upande wa utetezi ambao unaongozwa na mawakili wawili ambao ni Alfred Mwakingwe akisaidia na Jackson Chaula waliiomba Mahakama hiyo kumuachia kwa dhamana kwa sababu kosa linalomkabili mtuhumiwa linaruhusu kupewa dhamana.