Maonyesho ya kimataifa ya madini ya Vito Arusha Gem Fair yameanza leo jijini Arusha

0
128

Serikali ya Tanzania kwa kupitia Wizara ya nishati madini kwa kushirikia na chama cha wafanya biashara wa madini Tanzania TAMIDA leo wameanza rasmi maonesho ya sita kimataifa ya vito na  madini yenye lengo la kukuza Tanzania na kuifanya kuwa kitovu chabiashara ya  madini ya vito duniani.

IMG_20170503_110044

Akizungumza katika uzinduzi wa maonyesho hayo ambayo yanategemea kufanyika ndani ya siku tatu jijini Arusha Katibu wizara ya nishati na madini Prfesa JEMES MDOE amesema Tanzania imejaliwa kuwa na madini mbalimbali ya vito ambayo hupatikana nchini pekee kama tanzanite hivyo maonesho haya yana lengo la kuunganisha wanunuzi na wafanya biashara wa madini kutoka nchi mbalimbali duniani

IMG_20170503_110909

Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh Joel Bendera ambae pia ni mgeni rasmi katika maonesho hayo amesema ni fursa kubwa kwa maonesho haya kwasababu watu wanchi mbalimbali wanakuja kushiriki hivyo ni faida kwa watanzania na nchi kwa ujumla na pia wizara inafanya utaratibu wakuwa na senta ya kuongeza dhamani madini kwa mji wa mirerani ambapo madini pekee ya tanzanite yanapatikana

IMG_20170503_105316

Naye kwa upande wake mbunge wa simanjiro Ndg James Milya amesema pamoja na Tanzanite kupatikana pekee katika mji mdogo wa mirerani ila wananchi wa mji huo wanamaisha duni