CHAMA CHA WALI MKOANI (CWT) WILAYA YA KALAMBO CHA MBURUZA MAHAKAMANI MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO KWA KUSHINDWA KULIPA MADAI YAO

0
147

CHAMA walimu(CWT) katika  wilaya   ya  Kalambo  mkoani   Rukwa    kimemwandikia  barua  ya   kutishia kumshitaki  mkurugenzi  wa  halmashauri   hiyo  Saimoni   Ngahani  kwa madai   ya  kushindwa   kulipa  madeni  ya  walimu   kiasi   cha   shilingi  milioni  500.

Akiongea    wakati   wa  kikao  maalmu  na  viongozi  wa  chama  hicho  katibu  wa   chama  cha   walimu (CWT )   wilayani  humo   Pita   Simwanza, amesema wamefikia uamuzi huo baada ya   kujitokeza   kwa  malalamiko   kutoka  kwa  walimu ya kutolipwa   malimbikizo  ya  mishahara   yao  .

Akijibu malalamiko hayo,  Mkurugenzi  wa halmashauri hiyo ndugu Saimon  Ngaghani  amesema kuwa halmashauri haidaiwi na walimu bali kuna fedha za watumishi  SACCOS ambayo  iliingizwa kimakosa katika mfumo wa kifedha wa halmashauri na itarudishwa kwa wana SACCOS..