Nani zaidi kati ya Wakazi na Godzilla

0
142

Kituo cha runinga cha kimataifa cha MTV Base kimeingilia kati kufuta ubishi kati ya Godzilla na Wakazi wanaotambiana kwa uwezo wa utunzi wa mashairi na mtindo huru (Freestyle).

Mpaka sasa Wakazi anaongoza kwa asilimia 74% huku Godzilla akiwa na asilimia 26% ya kura 168 zilizopigwa huku yakiwa yamebakia masaa 14 kufungwa kwa zoezi hilo la upigaji kura.

Wakazi na Godzilla waliingia kwenye vita ya maneno wiki iliyopita kila mmoja akijinadi anauwezo wa kuandika mashairi zaidi ya mwenzake kitu ambacho kiliwapelekea kukutanishwa na kituo kimoja cha Radio jijini Dar es salaam na kushindanishwa ingawaje hakupatikana mshindi.

Baada ya mahojiano hayo rapa Wakazi aliona sio vizuri kupotezea kimya kimya akaingia studio na kutoa Diss Track kwa Godzilla aliyoipa jina la Zillnass.

Hata hivyo Godzilla nae akarudisha majibu na kutoa Diss Track yake kwa Wakazi aliyoipa jina la Power.