Kinana apiga marufuku uuzwaji fomu za uchaguzi CCM

0
28

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amepiga marufuku uuzwaji wa fomu za uchaguzi katika ngazi zote za uongozi na kama kuna mwanachama aliyeuziwa fomu arejeshewe fedha zake. Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM­Bara, Rodrick Mpogolo imesema kuwa Kinana amepata taarifa ya uuzwaji wa fomu za kuomba uongozi wa jumiiya katika ngazi ya wilaya, mkoa na Taifa jambo ambalo ni kinyume cha Katiba na kanuni za uchaguzi wa CCM. “Kwa kuepuka kujenga matabaka baina ya ‘walionacho’ na ‘wasionacho’ ndiyo maana kanuni za uchaguzi wa CCM hazikuruhusu jambo hili kufanyika.”