Kenya kuwania kuandaa mashindano ya Diamond league na Chipukizi wasiozidi miaka 20

0
27

Kenya imeelezea nia yake ya kuwania nafasi ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya dunia ya chipukizi wasiozidi miaka 20 mwaka wa 2020 na mkumbo wa kwanza wa riadha ya Diamond League muda mfupi baadaye.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya riadha ya chipukizi wasiozidi miaka 18 Jackson Tuwei, alifichua siku ya Jumatatu kwamba kamati yake ilifanya mazungumzo na rais wa shirikisho la kimataifa la riadha (IAAF), Sebastian Coe kuhusu uwenyeji wa matukio hayo mawili, na kupata majibu chanya kutoka kwa mkuu huyo.

Alisema mafanikio ya mashindano ya chipukizi wasiozidi miaka 18 yaliyokamilika siku ya Jumapili Nairobi imeipa kamati hiyo ujasiri kwa ajili ya matukio yoyote ya baadaye.