Mwanachama wa IAAF Frankie Fredericks asimamishwa kazi akisubiri uchunguzi

0
18

Mwanachama wa baraza la riadha duniani Frankie Fredericks amesimamishwa kwa muda kwa majukumu yake ya riadha kusubiri uchunguzi kuhusu uwezekano wa ukiukaji maadili. Haya yalifichuliwa na kamati hiyo siku ya Jumatatu.

Raia huyo kutoka Namibia anafanyiwa uchunguzi na kitengo cha uadilifu kuhusu malipo anayodaiwa kupokea kutoka Papa Massata Diack, mwanaye rais wa zamani wa IAAF Lamine Diack.

Inadaiwa kuwa mwanariadha huyo wa zamani alipokea malipo siku chache kabla ya kupiga kura kuhusu mwenyeji wa Olimpiki mwaka 2016. Lakini bingwa huyo wa medali ya Olimpiki kwa mara nne anasema malipo hayo yalikuwa halali kwani ilihusiana na nafasi yake katika kukuza matukio kadhaa ya riadha.