Afisa wa klabu ya Simba arejea kazini baada ya kuondolewa lawama

0
41

Mkuu wa kitengo cha habari cha klabu ya Simba SC ya Tanzania Haji Manara hatimaye amerejea kazini baada ya zaidi ya miezi miwili nje.

Minara alikuwa amepewa kifungo kama adhabu na kamati ya nidhamu ya TFF kwa siku zaidi ya 70 zilizopita baada ya TFF kumshutumu kwa kile kilichotaja kuwa kutoheshimu na kutofuata kanuni na maadili ya shirikisho hilo kama ilivyoainishwa kwenye kanuni zake.

Baada ya kuondolewa lawama, Manara alisema atafanya kazi yake kwa weledi, nidhamu na kuzingatia miiko ya mchezo wa soka.