Beki wa Taifa stars kukosa kiputwe dhidi ya Amavubi

0
18

Beki wa kulia wa timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars, Shomari Kapombe hakujumuishwa katika Kikosi cha stars kilichosafiri kuelekea Rwanda jumatano.

Stars itachuana na Amavubi katika mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya kufuzu mashindano ya CHAN itakayoandaliwa mwishoni mwa wiki hii katika Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.

Kikosi hicho cha Salum Mayanga ni lazima ishinde au kutoka sare ya zaidi ya bao moja hili ijikatie tikiti ya kuingia hatua ya pili ya mechi za kufuzu baada kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza wikendi iliyopita.