Kikosi cha wanabaiskeli kutoka Rwanda chashiriki mashindano Marekani

0
21

Timu ya taifa ya kuendesha baiskeli ya Rwanda ilianza jitihada yake ya kutwaa kombe la Cascade Cycling Classic jana usiku wakati waendeshaji hao walishiriki mashindano hayo ya kila mwaka kwa mara ya kwanza kabisa.

Timu ya Rwanda itashiriki mashindano hayo ambayo imepangwa Julai 19 hadi 23 kama maandalizi mashindano ya Colorado Classic itakayofanyika mwezi ujao.

Hii itakuwa mara ya kwanza kabisa kwa waendeshaji baiskeli kutoka Rwanda kushiriki mashindano ya Clorado Classic, ambayo imevutia timu ya UCI World Tour, UCI Professional continental team huku kikosi cha Rwanda kikiwa timu ya taifa ya pekee katika mashindano hayo yenye awamu nne.