Wadau waunga mkono hoja ya kubadili tarehe ya Kombe la Mataifa ya Afrika

0
21

Wadau wa soka sasa wameifisia hatua ya shirikisho la soka Afrika CAF kubadili tarehe ya mashindano ya mataifa bingwa barani Afrika, CAN.

Wadau hao, wakiwemo wachezaji, mawakala na wakufunzi wamedai kuwa hatua hii itawapa wachezaji kutoka Afrika nafasi nzuri kushindana na wenzao kutoka bara Ulaya. Aidha, kwa maoni yao, vilabu kubwa Ulaya watafurahi kwani hakuna mchezaji atayekosa mchezo wakati wowote wa msimu.

Kulingana na mabadiliko hayo, mashindano hayo sasa yatafanyika mwezi wa Juni na Julai kando na ilivyokuwa awali ambapo timu kutoka Afrika zilishiriki mashindano hayo mwezi wa Januari na Februari.

CAF pia imeongeza idadi ya timu zitakazoshiriki mashindano hayo kutoka 16 hadi 24