Serikali ya Uganda kutatua utata baina ya Micho na FUFA

0
22

Serikali ya Uganda huenda ikalazimka kuingilia kati na kumaliza mzozo unaoendelea baina ya Shirikisho la soka nchini Uganda FUFA na mkufunzi wa timu ya soka ya Uganda Cranes Micho Sredojevic.Hadi sasa FUFA imeshindwa kutoa mwelekeo kuhusu hatma ya kocha huyo ambaye anadai kuwa shirikisho hilo limeshindwa kumlipa malimbikizi yake ipasavyo.

Baada ya mkutano baina yake na mkufunzi huyo kutoka Serbia, FUFA ilikiri kuwa shirikisho hilo lina deni la kocha huyo japo halina fedha ya kutosha katika bajeti yake kuweza kumaliza deni hilo.

Ufichuzi huu umepelekea wadau wa soka nchini Uganda kuomba serikali kuingilia kati na kumaliza mzozo huo hili kocha huyo aendelee kutoa huduma zake kwa timu ya taifa ya Cranes ambayo inaendelea kutamba chini ya uongozi wake.