Nyota Novak Djokovic kutocheza tena 2017

0
28

Mshindi mara 12 wa Grand Slam Novak Djokovic hatashiriki mechi yoyote mwaka huu 2017 kutokana na jeraha la kiwiko.

Djokovic, aliyekuwa ameorodhesha nambari moja kwa mchezo wa tennis duniani, alijiondoa katika mashindano ya Wimbledon katika hawamu ya robo fainali kwenye muchuano dhidi ya Tomas Berdych Julai 12.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, alidai kuwa amekuwa akiuguza jeraha la kiwiko kwa miezi 18 na hangestahimili maumivu wakati wa mechi.

Raia huyo wa Serbia anayeorodheshwa nambari nne anasema atatumia muda wake sasa kuinua hali ya mwili wake pamoja na kushughulikia sehemu ya mchezo wake ambao anasema inahitaji kuboreshwa.