Tetesi za usajili wa soka Ulaya

0
92

Mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, mwenye miaka 18, ameamua kuondoka klabu hiyo huku Real Madrid, Manchester City na Paris Saint-Germain zikipambana kumsajili. Barcelona tayari wamewasiliana na Monaco kuhusu Kylian Mbappe.Ligi ya Uhispania haitokubali kupokea malipo ya kutengua kifungu cha uhamisho wa Neymar kutoka PSG kwa sababu ya mzozo wa malipo ya uzalendo kati ya Neymar na Barca na pia wasiwasi kuhusu PSG kukiuka kanuni za fedha za UEFA. UEFA itaitaka PSG kujieleza jinsi inavyopanga kupata fedha za usajili wa Neymar.

Manchester United wapo tayari kumpa nafasi katika kikosi cha kwanza kiungo chipukizi Scott McTominay. Jose Mourinho amesema mshambuliaji Anthony Martial, 21, haondoki Manchester United licha ya kuhusishwa na kuhamia Inter Milan. Meneja wa Tottenham anataka kumfanya kipa Paulo Gazzaniga, 25, kuwa usajili wake wa kwanza kwa kutoa pauni milioni 2 kwa Southampton. Meneja wa Atletico Madrid Diego Simione ameiambia bodi ya klabu yake kuwa lazima wamsajili Diego Costa, 28, ambaye Chelsea wanasema anauzwa kwa pauni milioni 50. Chelsea nao hawana haraka ya kumuuza Diego Costa, na wamedhamiria kushikilia bei ya pauni milioni 50. Pia inatazamia kumsajili kiungo wa Leicester Danny Drinkwater, badala ya Renato Sanches, wa Bayern Munich.