Polisi waua 13 Kibiti, wakamata silaha nzito

0
38

Jeshi la Polisi Jeshi la Polisi limedai kuwaua watu 13 wanaotuhumiwa
kufanya mauaji wilayani Kibiti mkoani Pwani na limekamata bunduki nane, magazini
mbili, risasi 158, mabomu manne, pikipiki mbili, vitenge na begi.
Taarifa ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro iliyotolewa jana imeeleza kuwa
Agosti 4, katika eneo la Gari Bovu, Kijiji cha Chamiwaleni wilayani hapo polisi
walimkamata Abdallah Mbindimbi Abajani akiwa ana majeraha maeneo mbalimbali ya
mwili wake akionekana kuwa alikuwa anaendelea kujitibu mwenyewe kwa kificho.
Alisema alipohojiwa kuhusiana na tuhuma zinazomkabili, alikubali na alionyesha dhamira
ya kwenda kuonyesha ngome yao.
Alisema juzi katika mapori ya Kijiji cha Rungungu, mtuhumiwa huyo aliwaonyesha polisi

source:Mwananchi