Waangalizi wasaka suluhu na timu ya Raila Odinga Kenya

0
72

Waangalizi wa kimataifa wa Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Madola
wametoa ripoti zao za awali kuhusu uchaguzi Kenya na mazungumzo yao na kambi ya
upinzani ya National Super Alliance (Nasa) iliyowasilisha madai kwamba kompyuta za
Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ziliingiliwa na upande Jubilee ili kuvuruga matokeo
ya kura.
Kiongozi wa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Afrika, Thabo Mbeki alisema mgombea
wa Nasa, Raila Odinga na ujumbe wake walikutana nao wakiwa na nyaraka za madai
kuhusiana na Jubilee kuvamia kompyuta hizo.
Mbeki alisema waliwasikiliza na kuwaeleza kuwa watalifikisha suala hilo IEBC. Hata
hivyo, alisema Nasa walitaka waangalizi hao wazifanyie kazi nyaraka hizo.