”Dele Alli Hauzwi hata kwa dawa ” Daniel Levy

0
34

Afisa Mkuu wa Tottenham, Daniel Levy ametangaza marufuku ya klabu hiyo ya kumuuza mshambuliaji wao, Dele Alli kwa gharama yoyote ile hata likitangazwa dau la Pauni 150 milioni kutoka klabu za Barcelona na Manchester City ambazo zinamuwinda.Mashabiki wa klabu hiyo nao wameingiwa hofu baada ya kuwapo taarifa za beki Danny Rose kutaka kutimkia Chelsea katika dirisha la usajili la kiangazi kabla halijafungwa.

Alli mwenye miaka 21 amekuwa miongoni mwa wachezaji chipukizi duniani, huku klabu vigogo barani Ulaya zikimuwinda kabla ya dirisha la usajili kufungwa Agosti 31.