Jose Mourinho atoa darasa kwa wachezaji wake

0
22

Kocha Jose Mourinho amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanajipanga vyema ili kutwaa taji la Ligi Kuu England na Kombe la FA na kufikiria angalau kufika nane bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mourinho aliwakumbusha wachezaji hao kuendeleza ari ya ushindi kutokana na kuweka rekodi nzuri ya kufunga mabao 4-0 katika mechi yao ya kwanza ya ufunguzi Ligi Kuu England ambayo haijawahi kufikiwa kwa mika 18 iliyopita.

Kocha huyo aliwataka wachezaji wake kufanya makubwa kwenye msimu, huku akizungumzia kuwa kampeni yake ilikuwa ni kushinda mechi zote za kabla ya msimu jambo ambalo wamelifikia kwa kiasi fulani.