Simba SC wakabidhiwa Ngao ya Jamii 2017

0
352

Klabu ya Simba SC imechukua ubingwa wa Ngao ya Jamii 2017 kwa mikwaju ya penati dhidi ya watani wao wa jadi Yanga SC katika mchezo uliochezwa jana Jumatato ndani ya dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Wekundu hao wa Msimbazi wamechukua ubingwa baada ya kushinda penati 5 kwa 4 kati ya penati 6 zilizopigwa

Mchezo huo ulianza kwa vuta nikuvute mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza mpira ulimalizika bila timu hizo kufungana huku beki wa wekundu hao, Method Mwamjale akipewa kadi ya njano katika dk 35 ya mchezo baada ya kuonyesha nidhamu mbaya kwa mwamuzi wa mchezo huo, Elly Sasii.

Katika kipindi cha pili mchezo ulianza kwa kasi kila mmoja akitaka kuona nyavu za mwenzake bila mafanikio huku kila mmoja akionekana kumkamia mwenzake hali iliyopelekea mchezo huo kamalizika bila kufungana na kuingia kwenye mikwaju ya penati iliyohitimisha kwa kuwatoa kifua mbele Wekundu wa msimbazi.