Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA lachezesha droo ya hatua ya makundi

0
337

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA jana ilichezesha droo ya hatua ya makundi ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2018 huko mjini Monaco Ufaransa. Katika droo hiyo klabu ya Tottenham itavaana na mabingwa watetezi wa kombe la vilabu bingwa Ulaya Real Madrid katika awamu ya kimakundi ya kombe hilo.

Spurs wao wamewekwa katika kundi H pamoja na Real Madrid, Mabingwa wa Ujerumani Borussia Dortmund na Apoel ya Urusi.

Droo hiyo inamuweka winga wa Real Madrid Gareth Bale na klabu yake ya zamani Tottenham. Bale alihamia Real Madrid kutoka Tottenham 2013. Mabingwa wa Uskochi Celtic wanakabiliwa na kibarua kigumu katika kundi moja na Bayern Munich , PSG na Anderlecht.

Mabingwa wa Uingereza Chelsea wamewekwa katika kundi moja na Atletico Madrid, Roma na Qarabag katika kundi C, huku mabingwa wa kombe la Yuropa Manchester United wakikabiliana na Benfica, Basle na CSKA Moscow katika kundi A.

Manchester City watamenyana dhidi ya Shakhtar Donetsk, Napoli na Feyenoord katika kundi F huku liverpool ikikabiliana na Spartak Moscow, Sevilla na Maribor katika kundi E.