Arsenal yaendeleza uteja kwa Liverpool

0
199

Majogoo wa Anfield Liverpool wameutumia vyema uwanja wao wa nyumbani kwa kuichapa Arsenal mabao 4-0.Mbrazil Roberto Firmino alianza kuipatia timu yake bao la 1 katika dakika ya 17, katika dakika ya 40 Sadio Mane akaongeza bao la 2.

Katika kipindi cha pili Mohamed Salah akawamsha tena mashabiki wa liverpool kwa bao la 3 kisha Daniel Sturridge akahitimisha kazi kwa bao la 4.

Bingwa mtetezi Chelsea walichomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton, nayo Tottenham Hotspur wakashindwa utumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kukubali sare ya bao 1-1 na Burnley.