Bei ya mbaazi yakatisha tamaa wakulima mkoani manyara

0
586

BABATI

Wakulima wa zao la mbaazi mkoani manyara wamelalamikia kuporomoka kwa soko la zao hilo mkoani humo.

Wakizungumza mkoani humo wamesema kuwa wao kama wakulima wanavunjika moyo wanapoona bei ikizidi kushuka kwani  kwa sasa  kilo moja ya mbaazi inanunuliwa kati ya shilingi 300 na 400 tofauti na mwaka jana kilo iliuzwa kwa shilingi 2,000 mpaka 2,500.

Wamesema kuwa licha ya Tanzania kuwa na maeneo makubwa ya uzalishaji wa mazao ,bado juhudi za kimasoko hazijafanywa kuwasaidia wananchi.

Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa idara ya kilimo na washirika DANIEL LUTHER amewataka wakulima wa zao la mbaazi mkoani Manyara kulitumia zao hilo kama zao la chakula badala ya kulifanya  zao la biashara kwani bado mazingira ya soko lake hayajawa ya uhakika.