Jeshi la polisi mkoani Arusha limethibitisha vifo vya watoto wawili waliokuwa wametekwa

0
97

Jeshi la polisi mkoani Arusha limethibitisha vifo vya watoto wawili ambao walikutwa wakiwa wamefariki dunia eneo la Olasiti jijini hapa,mara baada ya kutekwa,na kijana mwenye umri wa miaka 18 na kisha kutupwa katika kisima cha maji huku miili yao ikikutwa ikiwa imeharibika.

Akitoa taarifa hizo kwa wandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha Kamanda Charles Mkumbo ameeleza kuwa siku ya jana jeshi la polisi kwa kushirikiana na mtuhumiwa wa utekaji huo wa watoto aliyefahamika kwa jina la Samson Peter mwenye umri wa miaka 18 waliweza kufika katika nyumba moja jijini hapa ambapo palikuwa na kisima kirefu kwa ajili ya chemba sehemu ambayo watoto Mourn Ernest mwenye umri wa miaka sita na Ikramu Salum mwenye umri wa miaka mitatu walikutwa wakiwa wamefariki dunia.

Pamoja na kueleza juu ya tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa ameeleza jinsi walivyoweza kumkamata kijana huyo.

Kwa upande wake mama mwenye nyumba walipokutwa marehemu hao,pamoja na babu wa watoto hao waliweza kuzungumzia tukio hilo pamoja na kueleza masikitiko yao.

Mnamo siku ya tarehe 21 mwezi wa nane mwaka huu watoto wanne waliweza kutekwa na watu wasiojulikana huku watu hao wakidai kiasi kikubwa cha fedha kuwaachia watoto hao.

Wakati huo huo jeshi la polisi mkoani Arusha limethibisha tukio la uporaji wa fedha majira ya saa kumi na moja jioni mkoani hapa kwa mhasibu wa kampuni ya utalii ya Leopad ambaye aliporwa kiasi cha shilingi million 117 na watu wasiojulikana.