Mkuu wa Wilaya ya Babati azitaka taasisi za Elimu kuweka wazi matumizi ya ruzuku

0
31

Mkuu wa Wilaya ya Babati  Mkoani Manyara,Raymond Mushi amezitaka idara za elimu wilayani humo kutumia fedha za ruzuku na za umma zinazotolewa na serikali shuleni kwa kufuata mwongozo wa elimu na kuacha kufanya  siri katika matumizi ya fedha hizo.

Akizungumza wakati wa kuzindua wa mradi wa ufuatiliaji wa raslimali za umma(PETS) unaotekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la  Haki Elimu na Marafiki wa Elimu alisema viongozi wanapaswa kuweka wazi ripoti ya fedha ili kuondoa utata wa kuhoji matumizi ya ruzuku zinazotolewa.

Naye Mratibu wa shirika la Haki Elimu, Godfrey Boniventura alisema kutokana na uwepo wa tatizo la matumizi yasiyo sahihi  ya fedha na yasiyofuata mwongozo unaotolewa  katika sekta ya elimu shirika hilo limefanya utafiti mdogo  katika shule 15 za msingi na shule 10 za sekondari katika wilaya za Babati Mji na Wilaya.

Marafiki hao wa elimu wapatao  elfu 40 ambapo kwa wilaya ya Babati wapo 40  ni watu wanaolenga kuboresha elimu wamejengewa uwezo  katika kuwiwa kuboresha elimu ya msingi na sekondari chini ya Haki Elimu na kuleta mabadiliko chanya katika elimu.