MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU AZINDUA MAKUMBUSHO MAPYA YA OLDUVAI GORGE

0
33

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amezindua makumbusho ya Olduvai Gorge, ambako ni chimbuko la historia ya binadamu.

4

 Amesema makumbusho hayo ni kielelezo cha maisha na ustaarabu wa binadamu ambao unaelezea maisha ya vizazi vilivyopita. Amesema ujenzi wa makumbusho hayo utasaidia kuvutia watalii na wanasayansi wa masuala ya mambo kale duniani.

 Samia amesema eneo la Ngorongoro lina historia kubwa ya maisha ya zamadamu ikibainika miaka 3 milioni iliyopita walikuwepo walioishi kwa kutembelea miguu miwili.

 Amesema eneo la Ngorongoro kumebainika miaka 2.7 milioni iliyopita binadamu walianza kutumia zana za mawe katika kula nyama na kuwinda. Makamu wa Rais ameishukuru Jumuiya ya Ulaya kwa kutoa fedha kugharimia ujenzi wa makumbusho hayo na miundombinu yake.

 Meneja wa idara ya urithi wa tamaduni katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mhandisi Joseph Mwankunda amesema ujenzi wa eneo hilo umegharimu Sh1.7 bilioni.