BARABARA ,MAJI NI MIRADI ILIYO LETA MATUMAINI KWA WAKAZI WA BABATI

0
19

Licha  ya wakazi 3100 wa Kijiji cha Boay Wilayani Babati Mkoani Manyara  kunufaika na mradi wa Barabara  wa Mela –Bonga yenye urefu wa km 88.8 wananchi hao pia wamenufaika na Mradi wa maji  uliogharimu shilingi  milioni 42.63.

 Akipokea mradi huo kutoka kwa kampuni ya  China Road Seventh Group (CRSG) ambao ndio walikuwa wajenzi wa Mradi huo wa barabara,  Meneja wa TANROADS Mkoa wa Manyara Bashiru Rwesingisa  Amesema ujenzi wa kisima hicho ni makubaliano kati ya Tanroads na Mkandarasi wa Barabara hiyo .

 Alisema kuwa pindi ujenzi unapokamilika visima hivyo vitakabidhiwa rasmi kwa wananchi hasa wa maeneo yenye ugumu wa kupata maji .

 Alitaja visima vingine vilivyochimbwa  na Mkandarasi ni Kijiji cha Ukung’uku,Kijiji cha Kolo ambapo kilikarabatiwa na kuwekwa  pampu mpya, visima viwili  katika Kijiji cha Masawi na kisima kimoja katika Kijiji cha Bereko vyote vipo  Wilayani Kondoa.