KESI YA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA YA MASOGANGE YAPIGWA KALENDA

0
60

Video Qeen, Agnes Gerald maarufu kama Masogange akitoka katika mahakama ya  Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kusomewa mastaka yanayomkabiri ya
matumizi ya Dawa za kulevya na kesi yake kupigwa Kalenda mpaka Novemba
14, 2017.

Video Qeen, Agnes Gerald maarufu kama Masogange akizungumza na wakili Rouben  Semwanza leo mara baada ya kufika katika mahakama ya hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeipiga kalenda kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili  (Video Qeen), Agnes Gerald maarufu kama Masogange hadi Novemba 14 mwaka huu ambapo shahidi wa upande wa utetezi atatoa  ushahidi wake.

Mshtakiwa Masogangea alipaswa kuanza kujitetea leo
lakini wakili wa Serikali, Adolf Mkini aliomba  kwa Hakimu Mkazi Mkuu,
Wilbard Mashauri kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine.

Masogange  ataanza kujitetea baada ya mahakama kumkuta na  kesi ya kujibu kwa  upande wa mashtaka kuleta mashahidi watatu na kuufunga kesi, Masogange  pia anatarajia kuita mashahidi watatu.

Masogange anadaiwa kuwa  kati ya Februari 7 na 14,2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam  alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety  Imophine).

Pia anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017  alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.