MTUKUFU AGA KHAN KUHITIMISHA ZIARA YAKE LEO

0
29

Kiongozi wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, Mtukufu Aga Khan anatarajiwa kuondoka leo baada ya kuwasili  nchini jana akitokea Uganda  kwa mwaliko wa Rais John Magufuli.

Mtukufu Aga Khan aliwasili  jana Jumatano saa nne asubuhi na alipokewa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,  Dk Hussein Mwinyi na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.

Baada ya kushuka kwenye ndege, Mtukufu Aga Khan alikagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Polisi na kutazama burudani ya vikundi vya ngoma.

Kiongozi huyo amekuwa na mazungumzo na Rais Magufuli mchana huu na kesho atahitimisha ziara nchini.