UKOSEFU WA UZIO HUSABABISHA UVAMIZI WA WANYAMA WAKALI SHULE YA SEKONDARI TINGATINGA

0
37
Picha na maktaba ya google

SHULE ya Sekondari ya Tingatinga, Wilayani Longido, imeomba serikali na wadau wa elimu kuwajengea uzio ili kujikinga na wanyama wakali wakiwemo Tembo wanaofika shuleni hapo na kuhatarisha maisha ya waalimu na wanafunzi.

 

Akizungumza  katika Mahafali ya tatu ya wahitimu 185 wa kidato cha nne, Mwalimu Mkuu wa Sekondari hiyo, Pantaleo Paleso alisema ukosefu wa uzio shule hiyo iliopo katikati ya Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) na hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA), kunasababisha taharuki ya kila mara kwao hasa kipindi cha kiangazi.

 

Kwa upande wa wahitimu katika risala yao iliyosomwa na Veila Laurence, alisema upungufu wa vifaa vya matibabu husababisha wanafunzi wanapougua kukosa huduma stahiki za afya na hulazimika kuacha masomo na kwenda nyumbani kwa matibabu.

 

Mkuu wa Wilaya ya Longido,Daniel Chongolo aliwahakikishia kulifanyia kazi suala la ukamilishaji vyumba viwili vya maabara, mabweni,Nyumba za waalimu, barabara ya lami na uzio ilo waweze kusoma kwa usalama zaidi ya sasa.